HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na JB Nateleng
Kama njia moja wepo ya kutunza na kuhifadhi mazingira ya ziwa Turkana, viongozi wa Kitengo cha Usimamizi wa Ufuo (BMU) ya Moite Eneo wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit wameanzisha zoezi la kusaka nyavu ambazo zilikuwa zimeharamishwa kutumika katika ziwa hiyo..
Kulingana na Andrew Dokoya ambaye ni mwenyekiti wa usimamizi wa ufuo ya Moite, na pia katibu wa muungano wa Lake Turkana BMU Network ni kuwa waliweza kuzuru maeneo ya Napak, Lomanimania, Kasarakin, Naingol, Nariamawoi, Lotuku,Lotasia hadi Losibitar ili kuendeleza msako wa nyavu aina ya Monofilament net ambayo inaathiri mfumo wa uvuvi katika eneo la Moite.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Andrew amesema kuwa waliweza kufanikiwa kuchoma asilimia kubwa ya nyavu hiyo katika maeneo kadhaa Moite.
Andrew amesema kuwa nyavu hiyo pia imechangia katika upungufu wa samaki baharini kwani inafua mpaka samaki wale ndogo ambazo si halali kuzivua.
Andrew ametoa wito kwa serekali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kuwasaidia na kuwafadhili ili kuhakikisha kuwa zoezi hili limeboreshwa kwa manufaa ya jamii ambayo wanatumia ziwa kama kitega uchumi chao.