Featured Stories / News

MAANDAMANO YA GEN Z KAUNTI YA MARSABIT YAKOSA KUFANYIKA KUTOKANA NA MPANGO WA WAHUNI KUINGILIA KATI ZOEZI HILO.

Na Caroline Waforo Maandamano ya Gen Z kaunti ya Marsabit yalikosa kufanyika hii leo kutokana na taarifa za kuingiliwa na wahuni kwa nia ya kusababisha uharibifu wa mali. Kulingana na Kamanda wa kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo kunao wahuni waliopanga kuvuruga maandamano hayo na kusababisha uharibifu. Kamanda Kimaiyo anasema kuwa[Read More…]

WATU WANAOISHI KARIBU NA MSITU MARSABIT WATAKIWA KUJIANDIKISHA KUWA WANACHAMA WA COMMUNITY FOREST ASSOCIATION

NA GRACE GUMATO Shughuli ya kuhamasisha jamii wanaoishi karibu na msitu na kuisajili kamati mpya itakayosimamia jamii katika maswala ya misitu inaendelea katika lokesheni mbali mbali  katika eneo bunge la Saku katika kaunti ya  Marsabit. Kulingana na John Wako ambaye ni mwakilishi  wa jamii katika uhifadhi wa misitu  ni kuwa [Read More…]

WAANDAMANAJI MOMBASA WACHOMA MAGARI KADHAA BAADA YA WATATU KUPIGWA RISASI NA RAIA ALIYEKUWA NA BUNDUKI.

NA SAMUEL KOSGEI Waandamanaji wanaoipinga serikali jijini Mombasa walichoma magari na kuharibu hoteli baada ya mtu mmoja mwenye bunduki kufyatulia risasi ovyo umati wa watu na kuwajeruhi takriban watu watatu. Kulingana na walioshuhudia, mtu huyo anasemekana kukasirishwa na waandamanaji hao ambao walitatiza biashara katika Barabara ya Nyerere. Kufuatia hali hiyo,[Read More…]

ODM YATAKA SERIKALI IWAJIBIKIE MAUAJI, MAJERUHI NA UTEKAJI NYARA ULIOSHUHUDIWA NCHINI.

NA SAMUEL KOSGEI Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kinaitaka serikali ya Kenya Kwanza kuwajibikia mauaji, majeruhi na utekaji nyara ulioshuhudiwa nchini kufuatia maandamano ya Gen Z kupinga mswada tata wa fedha. Katika taarifa iliyosomwa na katibu mkuu wake Edwin Sifuna jijini Nairobi chama hicho kimeendelea kukashifu maafisa wa[Read More…]

WALIMU WA ECDE MARSABIT WAPOKEA MAFUNZO YA DIJITALI

NA SAMUEL KOSGEI Walimu wa shule za chekechea katika kaunti ya Marsabit wamepokezwa mafunzo ya kidijitali hatua ambayo inalenga kuwafaa wanafunzi 11 katika kaunti ndogo zote za Marsabit. Afisa mkuu katika idara ya elimu kaunti ya Marsabit Qabale Adhi alisema kuwa walimu wote wa ECDE watapokea mafunzo hayo ya kusomesha[Read More…]

HUDUMA ZA MAJI MJINI MARSABIT YAKATISHWA ILI KURUHUSU KUSAFISHWA KWA BWALA LA BAKULI 2 ULIOSAFISHWA MWISHO 1997

Na Samuel Kosgei KAMPUNI ya kushughulikia masuala ya maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO imeomba wakaazi wa mji wa Marsabit kuvumilia hatua ya maji kukatwa na kampuni hiyo siku nne zilizopita. Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Sora Katelo akizungumza na wanahabari katika bwawa la Bakuli ulio mlima Marsabit Jumatatu[Read More…]

Vijana wa Manyatta Ilman Chito wameamua kuchukua hatua na kuitaka Serikali ya Kaunti kushughulikia suala hili kwa haraka ili kuboresha maisha ya wakaazi wa eneo hilo .

NA JOHN BOSCO NATELENG Kundi la Vijana kutoka eneo la Manyatta Ilman Chito wadi ya Sagant Jaldesa wametoa rai kwa serekali ya Kaunti kuwakarabatia barabara ambayo imetatiza uchukuzi katika eneo hilo. Galma Iya ambaye ni mmoja wa Vijana hao amesema kuwa watu wa eneo hilo wamekuwa wakitatizika na ubovu wa[Read More…]

Subscribe to eNewsletter