Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Wakaazi wa Marsabit wamehakikishiwa kuwa bima ya afya ya SHIF inafanya kazi ipasvyo.
Akizungumza na idhaa hii alipokuwa akizuru hospitali ya rufaa ya Marsabit maneja wa mamlaka hiyo ya afya ya jamii (SHA) Lawrence Mutuma amewahakikishia wakaazi kuwa wagonjwa wa figo wanapata hudumu ipaswavyo kando na changamoto ya kujisajili na mfumo huu mpya ya SHA.
Aidha Musa Omar Guyo mmoja wa wagonjwa wanaopata matibabu ya figo katika hospitali rufaa ya Marsabit amesema kuwa kando na changamoto ya usajili amelezea kuwa SHA ikilinganishwa na NHIF ni afadhali kwa malipo.
Jamal ambaye pia ni mmoja wa wagonjwa wa figo anaelezea kuwa ni vyema kila mmoja ambaye ana magonjwa sugu kujisajili kwa bima ya SHA ili apate huduma kwa gharama nafuu.