Local Bulletins

MWANAUME MWENYE MIAKA 27 ASHTAKIWA MAHAKAMA YA MARSABIT KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO WA MIAKA 2 NA MIEZI 9.

 NA CAROLINE WAFORO

Mwanaume moja wa umri wa miaka 27 ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kumnajisi mtoto wa miaka miwili na miezi 9.

Inaripotiwa kuwa mnamo tarehe 21 mwezi juni mwaka 2024 mtuhumiwa Umuro Roba Dalana alimnajisi mtoto huyo mdogo katika eneo la Manyatta Bubisa kaunti hii ya Marsabit.

Umuro alifikishwa mahakamani mbele ya hakimu SK Arome mnamo tarehe 24 mwezi uo huo wa Juni. Aidha upande wa mshtakiwa ulidai kuwa mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya kiakili kutokana na ajali ya barabarani aliyopata mwaka 2019.

Mahakama iliagiza afanyiwe uchunguzi katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ambapo amepewa rufaa hadi katika hospitali ya rufaa ya  Mathari kaunti ya Nairobi.

Kesi hiyo imetajwa tena leo tarehe 3 mwezi juni ambapo mahakama imeamuru mtuhumiwa kupelekwa katika hospitali hiyo ya mathari kwa uchunguzi chini ya ulinzi wa maafisa wa usalama.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 4 mwezi 9 mwaka huu.

 

Subscribe to eNewsletter