Local Bulletins

HUDUMA ZA MAJI MJINI MARSABIT YAKATISHWA ILI KURUHUSU KUSAFISHWA KWA BWALA LA BAKULI 2 ULIOSAFISHWA MWISHO 1997

Na Samuel Kosgei

KAMPUNI ya kushughulikia masuala ya maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO imeomba wakaazi wa mji wa Marsabit kuvumilia hatua ya maji kukatwa na kampuni hiyo siku nne zilizopita.

Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Sora Katelo akizungumza na wanahabari katika bwawa la Bakuli ulio mlima Marsabit Jumatatu alisema kuwa maji yamekatwa kwa wateja wote mjini Marsabit na viunga vyake kutokana na mchanga na uchafu mwingi katika bwawa hilo la bakuli 2.

Sora alisema kuwa bwawa hilo kwa sasa linasafishwa kwa mchanga kuondolewa ili maji yaweze kutiririka vyema yanapopigwa na mashine kinyume na ilivyo kwa sasa ambapo mchanga inazibia mifereji muhimu.

“Tunasikitika kuambia wananchi wetu kuwa hawatakuwa maji kwa muda wa wiki moja kwa sababu ya kazi inayoendelea. Hii kazi ya kutoa uchafu katika bakuli 2 sio rahisi” Alisema Sora

Sora wakati uo huo alisema kulikuwa na haja kubwa sana ya kuondoa mchanga katika bwawa hilo kutokana na gharama kubwa inayoongezeka kutokana na kero hilo.

Anasema kuwa bwawa hilo mwisho lilisafishwa mwaka wa 1997 na hvyo kutaka wateja wao wa maji kuwapa muda wa wiki moja kukamilisha zoezi hilo kwani linafanywa kwa njia mikono.

Aidha alisema kuwa kampuni hiyo inalenga kununua jenereta ambayo itayapiga maji endapo umeme utapotea. Ameongeza kuwa wanatumia fursa hiyo kuyaongeza lita za maji yatakayopigwa kwa saa moja ili kutosheleza mahitaji ya wateja.

Shughuli yote hiyo inayojumuisha usafi, kurekebisha pampu na miradi mingine mbili Sora amesema itagharimu shilingi milioni karibia 5

Subscribe to eNewsletter