Local Bulletins

IDARA YA KILIMO JIMBONI MARSABIT YADHIBITISHA KUWEPO KWA NZIGE HUMU JIMBONI.

Na Caroline Waforo

Idara ya kilimo jimboni Marsabit imethibitisha kuwepo kwa nzige humu jimboni.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani naibu mkurugenzi wa kilimo jimboni Hassan Charfi amethibitisha hilo japo anaeleza kuwa nzige hao ambao wameripotiwa katika maeneo mengi jimboni Marsabit ni ‘nzige-miti’ yaani tree locust na wala sio nzige wa Jangwani yaani Dessert Locust.

Anasema nzige hao ni tofauti kwani Nzige-miti wanapatikana sana mitini na husabaisha uharibifu wa miti na hata mimea.

Nzige wa Jangwani wanapatikana wakiwa wengi sana na hujikusanya katika makundi makubwa na kusafiri umbali mkubwa.

Kulingana na Charfi nzige wa Jangwani ni waharibifu kuliko wale nzige-miti kwani huvamia mimea na majani na kutishia kuathiri uzalishaji wa chakula japo wote wanathibitiwa kutumia mikakati sawa.

Vile vile Charfi amedokeza kuwa wanashirikiana na idara ya serikali kuu kuhusu kilimo ili kupata kemikali za kukabiliana na nzige hao wasumbufu.

Subscribe to eNewsletter