Local Bulletins

Vijana wa Manyatta Ilman Chito wameamua kuchukua hatua na kuitaka Serikali ya Kaunti kushughulikia suala hili kwa haraka ili kuboresha maisha ya wakaazi wa eneo hilo .

NA JOHN BOSCO NATELENG

Kundi la Vijana kutoka eneo la Manyatta Ilman Chito wadi ya Sagant Jaldesa wametoa rai kwa serekali ya Kaunti kuwakarabatia barabara ambayo imetatiza uchukuzi katika eneo hilo.

Galma Iya ambaye ni mmoja wa Vijana hao amesema kuwa watu wa eneo hilo wamekuwa wakitatizika na ubovu wa Barabara hiyo kwani kwa muda sasa serekali haijaweza kukarabati barabara hiyo.

Galma ameeleza kuwa imekuwa vigumu kuwasafirisha wagonjwa pamoja na  wamama wajawazito kufika hospitalini kupata matibabu kwa sababu ya hiyo barabara.

Galma amewataka wakazi wa eneo hilo kuungana na vijana ili kuhakikisha kuwa wamejiboresha badala ya kuwaongojea viongozi ambao wanachukua muda kuyatatua matatizo yao.

Bonaya Denge ambaye ni kiongozi wa vijana katika eneo hilo amesema kuwa Kando na barabara bado eneo hilo halijapata umeme pamoja na maji kwa muda sasa na juhudi zao za kuwatafta viongozi na kuwaelezea shida yao ziliambulia patupu.

Subscribe to eNewsletter