Local Bulletins

NAIBU OCS WA KITUO CHA POLISI CHA DABEL, MOYALE AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI.

Na Silvio Nangori

Afisa mkuu wa polisi amefariki kwa kujitoa uhai alipojipiga risasi katika kituo cha polisi cha Dabel, Moyale, Kaunti ya Marsabit.

Inspekta James Moturi ambaye alikuwa naibu Afisa Mkuu wa Kituo (OCS) katika kituo cha polisi cha Dabel alijipiga risasi mita chache kutoka kwa kituo hicho cha polisi usiku wa kuamkia leo.

Akidhibitisha kisa hicho Kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kwamba afisa huyo alijipiga risasi kwenye kidevu.

Wenzake katika kituo hicho wamesema walisikia mlio wa risasi kutoka nyuma ya ofisi na walipokimbia kuangalia, wakapata Moturi amejipiga risasi.

Mwili wake umelazwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Moyale huku uchunguzi ukiendelea kwani hakuacha barua yoyote.

Visa vya maafisa wa polisi kujiangamiza zimekuwa zikiripotiwa humu nchini na kubainika kuwepo kwa msongo wa mawazo katika idadi kubwa.

Kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya polisi imezindua huduma za ushauri nasaha

 

Subscribe to eNewsletter