WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wahudumu wa afya wa kujitolea CHPs katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wametishia kuandamana iwapo serekali ya kaunti haitawalipa mishahara yao wa miezi minne.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wametaja kuwa hawajapokea mishahara ya mwezi Julai,Agosti,Septemba na Oktoba mwaka huu.
Wametaja kwamba hilo linalemaza kazi yao kutokana na kwamba wanahitaji data ili kuwasilisha kazi wanayoifanya kila siku.
Kwa upande wake mshirikishi wa huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Abdi Yusuf amewataka wahudumu hao wa afya wa kujitolea kuwa na subira kwani kuchelewa kwa mishahara yao kunatokana na kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za kaunti kutoka kwa serekali kuu.
Aidha Abdi ameweka wazi kuwa pia kubadilishwa kwa data za wahudumu hao wa afya haswa nambari za simu na akaunti za benki kama sababu nyingine inayochelewasha kulipwa kwa wahudumu hao wa afya wa kujitolea.