Local Bulletins

WAANDAMANAJI MOMBASA WACHOMA MAGARI KADHAA BAADA YA WATATU KUPIGWA RISASI NA RAIA ALIYEKUWA NA BUNDUKI.

NA SAMUEL KOSGEI

Waandamanaji wanaoipinga serikali jijini Mombasa walichoma magari na kuharibu hoteli baada ya mtu mmoja mwenye bunduki kufyatulia risasi ovyo umati wa watu na kuwajeruhi takriban watu watatu.

Kulingana na walioshuhudia, mtu huyo anasemekana kukasirishwa na waandamanaji hao ambao walitatiza biashara katika Barabara ya Nyerere.

Kufuatia hali hiyo, magari kadhaa yaliharibiwa na majeruhi walikimbizwa hospitalini.

Wazima moto, hata hivyo, walifanikiwa kuzima moto huo.

Subscribe to eNewsletter