Taylor Swift Unveils New Secret Double Album.
April 19, 2024
County updates, notifications, news from the Marsabit County
Na Samuel Kosgei Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Marsabit Peter Kihara amepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kufanyika katika uwanja na ukumbi wa kanisa Katoliki mjini Marsabit. Akizungumza alipoongoza misa ya sherehe ya Maria Consolata katika kathidrali ya Marsabit, Askofu Kihara alisema kuwa wema na ukarimu ambao umefanyiwa[Read More…]
Na Isaac Waihenya Serekali ya kaunti ya Marsabit inaandaa mikakati ya kuwaajiri walimu wa chekechea (ECDE) kwa mkataba wa kudumu. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Elimu katika kaunti ya Marsabit Bi. Ambaro Abdulla Ali. Akizungumza wakati wa kufunzu kwa zaidi ya walimu 230 wa shule za chekechea katika[Read More…]
Na Isaac Waihenya Wazazi katika eneo la Manyatta Jillo eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit, wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kutelekezwa na idara ya elimu hapa jimboni. Wakizungumza na vyombo vya habari wazazi hao walisema kuwa shule ya kipekee ya chekechea iliyopo katika eneo hilo imesalia na mwalimu mmoja[Read More…]
Na John Bosco Nateleng Askofu wa Jimbo hili askofu Peter Kihara amewashauri wanafunzi dhidi ya kujihusisha na wizi wa mitihani. Akihutubu katika shule ya wasichana ya Bishop Cavallera huko Karare wakati wa hafla ya kuwazawadi wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa KCSE mwaka jana, askofu Kihara alisema kwamba ni sharti[Read More…]
Na Jacob Nateleng Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Marsabit wamepongeza uteuzi wa Jumanne wa Kabale Tache Arero kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi-NLC, nafasi ambayo ameshikilia kama kaimu kwa miaka mitano iliyopita. Wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika eneo la Saku Abdi Boru wakazi hao[Read More…]
Na Isaac Waihenya Vijana wa klabu ya Soka ya Samba Boyz hapa mjini Marsabit wameirai jamii ya Marsabit pamoja na vilabu vingine kuwa katika mstari wa mbele kutoa damu ili kuokoa maisha ya wale wanaohitaji damu hiyo. Wakiongozwa na nahodha wao Siba Burcha vijana hao wametaja kwamba wamechukua jukumu la[Read More…]
Na Samuel Kosgei Aliyekuwa mbunge wa North Horr Chachu Ganya alipokelewa kwa shangwe na mbwembwe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA baada ya kurejea nchini akitokea Marekani alikotuzwa tuzo ya kimataifa ya marekani ya Sol Feistone aliyopewa baada ya jitihada zake za kuwasaidia watoto maskini zaidi ya 2000[Read More…]
Na Isaac Waihenya Mbunge wa Moyale Profesa Guyo Wako Jaldesa amedhibitisha kuwa ni kweli kuna baadhi ya wanafunzi katika eneo bunge lake wanaopewa hadi shilingi elfu 100,000 fedha za busari ya CDF. Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya Simu, mtunga sheria huyo alitaja kuwa hilo liliafikiwa kati yake na[Read More…]
Picha Silvio Nangori Na Silvio Nangori Hospitali ya Rufaa ya Marsabit hii leo imezindua mashine ya kuzalisha oksijeni ambayo inaweza kuzalisha mitungi 10 ya kilo hamsini ndani ya saa 24. Mashine hiyo ambayo imegharimu takriban milioni 20 imefadhiliwa na Shirika la Marekani la USAID. Katika hafla hiyo hospitali ya Rufaa[Read More…]
Na Silvio Nangori Mshukiwa wa wizi wa piki piki karibu na Shemeji inn katika eneo bunge la saku amefikishwa katika mahakama ya Marsabit. Inadaiwa kwamba Isaak Hussein Guracha alihusika katika wizi wa piki piki aina ya Skygo yenye nambari ya usajili KMGG 787P inayogharimu Sh 241,645 tarehe 5 Juni,2023 mali[Read More…]