HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Jalle Elias
Serikali imezindua zoezi la mafunzo ya kidijitali litakalo endelea kwa kipindi cha miaka miwili hapa jimboni Marsabit.
Kulingana na afisa wa mawasiliano katika mwavuli wa kaunti za FCDC Halima Golicha Ibrahim aliyezungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo ni kuwa majaribio ya zoezi hilo ambayo yamefadhiliwa na shirika la Raberry Pi Foundation yanalenga kuongeza maarifa ya kidijitali miongoni mwa wanafunzi na vijana ambao hawako shuleni.
Aidha Halima ameongezea kuwa wanalenga kuwapa mafunzo walimu 10 katika eneo la bunge la Saku.
Halima vilevile amewarai walimu kukumbatia mfumo wa kidijitali kwani kwa sasa ulimwengu unapiga hatua katika mambo ya kidijitali haswa kimasomo.