VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAMEITAKA JAMII KUZINGATIA MAADILI ILI KUEPUSHA VISA VYA MAUAJI VYA WANAWAKE NCHINI
November 5, 2024
Na Grace Gumato
Naibu msimamizi wa wa kituo cha Huduma Center hapa mjini Marsabit Diba Galgallo Bilala amekanusha madai kuwa kumekuwepo na visa vya ulaji hongo katika kituo hicho na kuyataja madai hayo kama yasiyo ya kweli.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake Diba amesema kuwa malipo yote katika kituo cha huduma Center yanapaswa kufanywa kupitia e-citizen ila si kwa njia ya kutoa pesa taslimu.
Diba ameweka wazi kuwa kuwa ada mpya za huduma zimeanza kutumika ambapo malipo cha cheti cha kuzaliwa ni shilling 450, kubadilisha kitambulisho ikiwa ni shiilingi 1200 na kwa cheti cha tabia njema kikitozwa shillingi 1200.
Hata hivyo Diba amesema kuwa yeyote ambaye ana malalamishi kuhusana na huduma zao basi anaweza kupiga ripoti kwa msimamizi wa kituo hicho ili kupata msaada.