WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Isaac Waihenya
Wazazi katika eneo la Manyatta Jillo eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit, wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kutelekezwa na idara ya elimu hapa jimboni.
Wakizungumza na vyombo vya habari wazazi hao walisema kuwa shule ya kipekee ya chekechea iliyopo katika eneo hilo imesalia na mwalimu mmoja pekee na ambaye wanahoji kuwa hawezi kuwapa mafunzo bora wanafunzi zaidi ya 120 waliomo shuleni humo.
Wazazi hao ambao waliandamana hadi katika ofisi ya waziri wa elimu hapa jimboni Marsabit kupeleka malalamishi yao, waliitaka serekali ya kaunti kusulushisha kero hilo ili watoto wao pia wapate elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Walisema kuwa hali ya shule hiyo pia ni ya kusiskitisha mno kwani watoto hao hawapati chakula kutoka kwa serekali na vilevile hawana choo.
Aidha Waziri wa Elimu katika kaunti ya Marsabit Bi. Ambaro Abdulla Ali ametaja kwamba wamepokea malalamishi yao na kuwa kuanzia Jumanne asubuhi watapata mwalimu mmoja zaidi.
Kuhusiana na swala la lishe kwa watoto hao wa chekechea waziri Ambaro alikariri kuwa hilo limeshughulikiwa huku akiahidi kwamba serekali ya kaunti inafanya kila iwezalo kutatua kero la walimu wa shule za chekechea hapa jimboni.