HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
NA EBENET APIYO
Shirika la mpango wa chakula ulimwenguni (WFP) limezindua rasmi programu ya chakula kwa watoto wa shule za chekechea (ECDE) katika kaunti ya Marsabit.
Masuala yaliyopewa kipaumbele kwenye uzinduzi huo ni pamoja na usalama wa chakula, biashara na uwekezaji na mwongozo wa utekelezaji wa sera za chakula.
Mkurugenzi wa kitaifa wa shirika hilo la (WFP) Lauren Landis akizungumza katika hafla hiyo amesema uzinduzi huo utawafaidi sana watoto wa chekechea kwani shule husika zitapokezwa vifaa kama vile; solar, vitabu na meko ya kupikia kama njia mbadala za kujifaidi.
Aidha waziri wa elimu hapa Marsabit Ambaro Ali Abdulahi, pia ametoa shukrani zake kwa shirika la mpango wa chakula ulimwenguni WFP kwa uzinduzi huo ambao utasaidia kuinua elimu jimboni.
Kadhalika Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Marsabit central David Saruni amesema kuwa chakula hicho kitawachochea watoto kuenda shule na pia kuwapunguzia mzigo wazazi ambao wanang`ang`ana kuwataftia wanao chakula.
Naye naibu gavana Solomon Gubo naye amesema kuwa kuna sera mwafaka za kuongoza elimu ya chekechea ili kufanikisha uwepo wa chakula salama kwa watoto wa shule za chekechea.