HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Carol Waforo
Idara ya usalama jimboni Marsabit imeongeza idadi ya maafisa wa polisi kushika doria katika mgodi wa Hillo ulioko eneo la Dabel eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.
Hili limethibitishwa na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo ambaye pia amedokeza kuwa wamewaondoa maafisa waliokuwa wakishika doria hapo awali.
Hii ni kufuatia kisa cha hivi maajuzi ambapo afisa mmoja wa polisi pamoja na raia waliaga dunia katika visa viwili tofauti kwenye machimbo hayo.
Katika kisa cha kwanza inaarifiwa kwamba maafisa wa polisi walifyatua risasi na kumuaa mwanamme mmoja katika makabiliano jambo lililotajwa kuchochea kisa cha pili ambapo wachimbaji migodi waliwashabulia maafisa wawili wa polisi muda mfupi baadae huku mmoja wa maafisa hao akikatwa shingo na kufariki papo hapo huku afisa wapili akinusurika.
Katika kisa hicho bunduki mbili aina ya G3 ziliibwa na wachimba migodi ambapo bunduki moja imepatikana hadi kufikia sasa.
Kulingana na afisa wa upelelezi kaunti ya marsabit Luka Tumbo bado wanaendeleza msako ili kuwakamata washukiwa waliohusika na mauaji ya afisa wa polisi pamoja na kusaka bunduki inayoaminika kuwa mikononi mwa wachimba migodi.
Tumbo pia amedokeza kuwa usalama umeimarishwa katika machimbo hayo.