County Updates, National News

Mtoto wa miaka 15 aaga dunia baada ya kusombwa na maji, Kargi, Marsabit

Na Isaac Waihenya

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 ameaga dunia siku ya Jumapili baada ya kusombwa na maji ya mto Kargi katika eneo la Kargi katika kaunti ya Marsabit.

Akidhibitisha kisa hicho MCA wa wadi ya Kargi Christopher Ogom amesema kwamba msichana huyo alikuwa akichunga mbuzi karibu na mto huo ila akasombwa na maji alipojaribu kuvuka wa upande wa pili.

Ogom ameweka wazi kuwa juhudi za wanakijiji kwa ushirikiana na naibu chifu wa eneo hilo Moses Galoro za kuokoa kijana huyo hazikufua dafu huku mwili wake ukiopolewa baadae.

Marehemu msichana huyo alizikwa jana jioni katika eneo la Hallam huko Kargi.

Ogom amelalamikia hali mbaya ya barabara sawa na kukosekana kwa daraja katika mto huo huku akisema kuwa hayo yanazua hudumu muhimu kufika katika eneo hilo kwani hakuna magari yanaingia wala kutoka eneo la Kargi.

Ogom amesema kuwa eneo hilo limekondolewa macho na hatari zaidi kuona kwamba wapo wagonjwa na ambao wanasaka matibabu zaidi ila wamekosa usaidizi kutokana na ubovu wa barabara huku akiitaka serekali ya kaunti sawa na ile ya kitaifa kuingilia kati ili kunasua hali.

 

Subscribe to eNewsletter