County Updates, Local Bulletins

Chachu Ganya Awasili Kutoka Marekani Alikotuzwa Tuzo ya Kimataifa Ya Sol Feistone

 

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Aliyekuwa mbunge wa North Horr Chachu Ganya alipokelewa kwa shangwe na mbwembwe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA baada ya kurejea nchini akitokea Marekani alikotuzwa tuzo ya kimataifa ya marekani ya Sol Feistone aliyopewa baada ya jitihada zake za kuwasaidia watoto maskini zaidi ya 2000 kwenye masomo yao katika ukanda wa kasakazni.

Akiwasili katika uwanja wa kimataifa wa JKIA Chachu aliahidi kuendeleza  kampeni yake ya kuwasaidia watoto maskini kwenye eneo la kaskazni na sehemu nyingine nchini akitumia pesa alizoshinda haswa katika ujenzi wa shule mbalimbali.

Alitoa wito kwa jamii za Marsabit kuzidi kuwapa elimu watoto wao kwani ndio njia pekee ya kukomboa jamii kutoka lindi la umaskini.

Subscribe to eNewsletter