KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya,
Mwenyekiti wa muungano wa baraza la makanisa tawi la Marsabit (NCCK)mchungaji Said Diba ametaja hoja ya kuwepo kwa mkao kati ya viongozi na vijana wa Gen Zs.
Mwenyekiti wa muungano wa baraza la makanisa tawi la Marsabit (NCCK)mchungaji Said Diba ametaja hoja ya kuwepo kwa mkao kati ya viongozi na vijana wa Gen Zs.
Akizungumza na vyombo vya habari, mchungaji Diba amesema kuwa ni muda mwafaka kwa vijana wa Gen Zs kuruhusu mazungumzo ili kuhakikisha kwamba maswala wanayoyaibua yanatatuliwa.
Mchungaji Diba hata hivyo ametaja kwamba ni jambo la kufedhehesha sana kuona kwamba maandamano ya vijana hawa yampata muingiliano kutoka kwa wahalifu jambo linalofuruga malengo yake.
Hata hivyo mchungaji Diba amepongeza hatua ya Rais Wiliam Ruto ya kuvunja baraza la mawaziri huku akiitaja kama ishara ya kuwa yupo tayari kupambana na ufisadi hapa nchini.
Vilevile amesifia kurejeshwa kwa mradi wa kazi kwa vijana unalenga kuwapa kazi vijana na kuwaepusha na kutumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa.