HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Caroline Waforo
Ajira kwa watoto imeongezeka katika kaunti ndogo ya Sololo eneobunge la Moyale kaunti ya Marsabit ambapo watoto wengi wanaaajiriwa katika kazi mbalimbali badala ya kuwepo shuleni.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu afisa wa kupigania haki za watoto katika shirika la Strategies for Northern Development (SND) Joan Chebet amesema kuwa wengi wa watoto hawa ni raia wa Ethiopia chini ya miaka 10.
Anasema kuwa kunazo kampuni ambazo zinawaleta hawa watoto nchini Kenya kuwatafutia ajira haswa ya kuwa wafanyakazi wa nyumba.
Aidha amedokeza kwua wanashirikiana na serikali ya Ethiopia ili kuwarejesha watoto hao nyumbani kwao kwani wengi wa wazazi wana ufahamu waliko wanao.
Ni visa ambavyo pia vimekaririwa na mwanaharakati wa kupigania haki za watoto Moyale Fathe Dika. Kulingana na Dika wamefanikiwa kuwanusuru baadhi ya watoto hao na kuhakikisha kuwa wanapata elimu.
Kadhalika ametaja kuwa visa vya ndoa za mapema vimeongeza katika eneo hilo hii ikitokana na mimba za utotoni.
Anasema kuwa wasichana wanaopata mimba za mapema wanalazimishwa kuolewa.
Haya yanajiri huku wazazi wakitakiwa kuwajibika katika malezi ya wanao huku wakaazi kwa ujumla wakitakiwa kuheshimu haki za watoto.
Wakti uo huoVisa vya ulanguzi wa binadamu haswa ulanguzi wa watoto vimetajwa kuongezeka kwenye mpaka wa Kenya na Ethiopia. Visa hivi vya ulanguzi vinatekelezwa kupitia mpaka wa Moyale kaunti ya Marsabit.
Chebet anasema kuwa watoto hawa pia wanatoka nchini Eritrea huku asilimia 80 ya watoto hao wakiwa wasichana huku akiweka wazi kuwa wamefanikiwa kuwarejesha watoto wote walionusuriwa kwa familia zao kule Ethiopia.
Vile vile Chebet anasema kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na serikali ya Kenya na ile ya Ethiopia ili kuhakikisha kuwa visa hivi vinapungua.
Umaskini umetajwa kuchangia pakubwa katika visa vya ulanguzi wa binadamu.Ulanguzi wa binadamu unaweza kuwa kwa aina ya kuwasafarisha watu kutoa taifa moja hadi lingine kiharamu kwa nia ya kuwatafuita ajira, kuwanyanyasa au hata kuwasajili katika makundi ya itikadi kali.