County Updates, Local Bulletins

Mbunge wa Moyale Profesa Waqo Jaldesa Adhibitisha Mpango wa Kutoa Basari Kufikia Sh100,000 Kwa Baadhi ya Wanafunzi, Moyale

PICHA: KWA HISANI

Na Isaac Waihenya

Mbunge wa Moyale Profesa Guyo Wako Jaldesa amedhibitisha kuwa ni kweli kuna baadhi ya wanafunzi katika eneo bunge lake wanaopewa hadi shilingi elfu 100,000 fedha za busari ya CDF.

Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya Simu, mtunga sheria huyo alitaja kuwa hilo liliafikiwa kati yake na kamati ya CDF katika eneo hilo ambapo kwa pamoja walikubali kuwafadhili wanafunzi wanaofanya kozi ambazo wanahisi ni muhimu mno katika jamii ya Moyale kwa ujumla.

Wanaonufaika na kiwango hicho cha fedha ni wanafunzi ambao hawana ufadhili wowote na wanaosomea kozi za Ualimu, Udaktari au matabibu, kozi za uhandisi na Sheria.

Professa Waqo alitaja kwamba hilo linalenga kuwapa motisha wanafunzi katika eneo hilo kusomea kozi hizo nne na kutia bidi masomoni.

Aidha Profesa Waqo alitaja kwamba kama eneo bunge wanalenga kutatua kero la ukosefu wa waalimu, madaktari, mainjinia na hata wanasheria, kero ambalo alisema kwamba kwa kipindi kirefu limeadhiri eneo bunge hilo.

Waqo vilevile ametaja kwamba hilo limewezeshwa pia na kuongezwa kwa mgao wa fedha unaoelekezwa kuwafadhili wanafunzi CDF kutoka shilingi milioni 21 miaka ya awali hadi shilingi milioni 55 mwaka huu, huku idadi ya wanaonufaika na mradi huo pia ikiongezeka maradufu.

Subscribe to eNewsletter