County Updates, Diocese of Marsabit

Askofu Peter Kihara Apiga Marufuku Mikutano Yote ya Kisiasa Katika Uwanja na Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mjini Marsabit

 

Askofu Peter Kihara | PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Marsabit Peter Kihara amepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kufanyika katika uwanja na ukumbi wa kanisa Katoliki mjini Marsabit.

Akizungumza alipoongoza misa ya sherehe ya Maria Consolata katika kathidrali ya Marsabit, Askofu Kihara alisema kuwa wema na ukarimu ambao umefanyiwa wanasiasa na asasi za uchaguzi kwa miaka mingi imeibuka kuwa kejeli na dharau kwa kanisa na mali ya kanisa katoliki Marsabit.
Amekariri kuwa si mara moja viongozi wanasiasa na wafuasi wao waliharibu mali ya kanisa na kukosa kulipia hasara suala analoseema kanisa halitavumilia katu.
Matokeo ya uchaguzi mkuu kiwango cha kaunti kwa miaka mingi yalikua yakitangaziwa ukumbi wa kanisa Katoliki mjini Marsabit.
Kauli yake Askofu Kihara inajiri majuma kadhaa baada ya mkutano wa chama cha UDA kushuhudia vurugu mwanzoni mwa mwezi huu, mkutano ambao uliandaliwa katika uwanja wa kanisa katoliki.

Subscribe to eNewsletter