Featured Stories / News

MAHAKAMA YA MARSABIT IMEMUHUKUMU KIFUNGU CHA MIAKA MIWILI GEREZANI MWANAUME MMOJA MWENYE UMRI WA MAKAMU KOSA LA KUPIGA MTU NA KUUMIZA.

Na Grace Gumato  Mahakama ya Marsabit imemuhukumu kifungu cha miaka miwili gerezani mwanaume mmoja mwenye umri wa makamu kwa kosa la kupiga na kuumiza mtu. Mshukiwa Kamau Kamotho anadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 mwezi huu almjeruhi vibaya mlalamishi Adan Isaak wakiwa mjini Marsabit eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.[Read More…]

BARAZA LA WAZEE WA JAMII YA GABRA LAITAKA SEREKALI KUHARAKISHA UCHUNGUZI KUHUSIANA MAUAJI YA ENEO LA ELLE-DIMTU AMBAPO WATU WANANE WALIUWAWA NA KISHA KUTEKETEZWA.

NA ISAAC WAIHENYA Baadhi ya wazee wa baraza la wazee wa jamii ya Gabra wamemtembea mmoja wa walionusurika katika kisa cha mauaji yaliyotekelezwa wiki jana na watu wasiojulikana katika eneo la Elle-Dimtu ambapo watu wanane waliuwawa na kisha kuteketezwa. Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Shama Boy Wario wazee hao[Read More…]

VIJANA WAWILI WAJERUHIWA KWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA ENEO LA KARANTINA, SAKU KAUNTI YA MARSABIT.

Na Talaso Huka Vijana wawili wamejeruhiwa usiku wa kuamkia leo baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Tukio hilo lilitokea eneo la Karantina, Saku kaunti ya Marsabit. Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa uchunguzi unaendelea huku akibainisha kuwa lengo la mavamizi hayo[Read More…]

VIONGOZI WA KISIASA NA WA KIJAMII KUTOKA MAENEO YA DUKANA, TURBI, MAIKONA NA NORTH HORR WAMEPEWA HAMASA KUHUSIANA NA NAMNA NA FAIDA ZA KUSAJILI ARDHI YA JAMII.

Na Isaac Waihenya, Viongozi wa kisiasa na wa kijamii kutoka maeneo ya Dukana, Turbi, Maikona na North Horr wamepewa hamasa kuhusiana na namna na faida za kusajili ardhi ya jamii katika kaunti ya Marsabit. Kwenye mkao ulioandaliwa hii leo na mashirika yasiyoyakiserekali ya IREMO na PISP ambao umewalata pamoja, MaMCAs wa[Read More…]

KAUNTI YA MARSABIT KUKUMBWA NA UHABA WA CHAKULA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MITATU IJAYO.

Na Grace Gumato, Mkurugenzi wa mamlaka ya kupambana na majanga NDMA kaunti ya Marsabit, Guyo Golicha amewathahadharisha wanaMarsabit kuhusiana na hatari ya uhaba wa chakula katika kipindi cha miezi mitatu ijayo. Akizungumza na idhaa hii afisini mwake Golicha amekariri kuwa kaunti hii itaweza kushuhudia hali ya ukame ambayo itasababisha upungufu wa[Read More…]

SEREKALI YATAKIWA KUINGILIA KATI,KUTATUA MASWALA YALIYOIBULIWA NA WALIMU ILI KUZUIA MGOMO ULIORATIBIWA KUFANYIKA MWANZONI MWA MUHULA UJAO.

Na Talaso Huka na Elias Jalle,  Serekali imetakiwa kuingilia kati na kutatua maswala yaliyoibuliwa na walimu ili kuzuia mgomo ulioratibiwa kufanyika mwanzoni mwa muhula ujao. Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa Chama cha walimu ya KNUT tawi la Marsabit Rose Mary Talaso ni kuwa hilo litahakikisha kwamba wanafunzi wataendelea na[Read More…]

VIONGOZI WA VIJANA,CHINI YA UONGOZI WA SHIRIKA LA YOUNG DREAMS WAANDAA KIKAO CHA KUTOA HAMASA KWA VIJANA WA ILLAUT KUHUSIANA NA SWALA LA MIMBA ZA UTOTONI.

Na Isaac Waihenya Kufuatia kisa cha hivi maajuzi ambapo mtoto wa siku moja alipatikana akiwa ametupwa katika shimo la choo katika kituo cha kibiashara cha Illaut Korr, viongozi wa vijana na wale wa serekali katika eneo hilo chini ya uongozi wa shirika Young Dreams wameandaa kikao cha kutoa hamasa kwa[Read More…]

HAKUNA VIJANA WALIOTENGWA KWENYE SHEREHE ZA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA. – ASEMA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA IFPC HASSAN MULATA.

Na Isaac Waihenya,  Mkurugenzi wa shirika la IFPC Hassan Mulata amekanusha madai kwamba kuna baadhi ya vijana waliotegwa katika sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana iliyoandaliwa katika shule ya upili ya Moi Girls hapa mjini Marsabit. Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee mulata ambaye alikuwa mmoja wa waandaaji wa hafla[Read More…]

Subscribe to eNewsletter