Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Caroline Waforo,
Watu watatu akiwemo mtoto wa miaka saba wanauguza majeraha baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuingia ndani ya nyumba ya makazi katika mtaa wa Shauri Yako wadi ya Marsabit Central kaunti ya Marsabit.
Mama na mwanawe wa miaka 7 walikuwa ndani ya nyumba hiyo wakati wa kisa hicho. Wamepata majeraha mabaya ya mikono na miguu.
Kulingana na kamanda wa trafiki kaunti ya Marsabit Jacob Kirop lori hilo lilipoteza mwelekeo baada ya breki kufeli.
Aidha dereva wa lori hilo mwenye umri wa miaka 35 pia alipata majeraha mabaya huku taniboi akinusurika bila ya majeraha.
Watatu hao wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Kamanda Kirop amewataka madereva kuwa makini barabarani na kuheshimu sheria za trafiki.