Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Baadhi ya wazee wa baraza la wazee wa jamii ya Gabra wamemtembea mmoja wa walionusurika katika kisa cha mauaji yaliyotekelezwa wiki jana na watu wasiojulikana katika eneo la Elle-Dimtu ambapo watu wanane waliuwawa na kisha kuteketezwa.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Shama Boy Wario wazee hao waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wakiwa katika hospitali ya Havanna hapa njini Marsabit ambapo mwadhiriwa amelazwa, wametaja kwamba mwadhiriwa yupo katika hali shwari huku akiendelea kupokea matibabu.
Aidha wamewataka wananchi kudumisha utulivu na kuwapa maafisa wa usalama nafasi ya kuendeleza uchunguzi ambao wamedai kwamba unafaa kukamilika haraka iwezekanavyo na waliotekeleza unyama huo wachukuliwe hatua kali za kisheria.