Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Isaac Waihenya
Kufuatia kisa cha hivi maajuzi ambapo mtoto wa siku moja alipatikana akiwa ametupwa katika shimo la choo katika kituo cha kibiashara cha Illaut Korr, viongozi wa vijana na wale wa serekali katika eneo hilo chini ya uongozi wa shirika Young Dreams wameandaa kikao cha kutoa hamasa kwa vijana kuhusiana na swala mimba za utotoni.
Wakiongozwa na Michael Lesagor vijana hao wamelitaja swala hilo kama lakufedhehesha mno huko akikariri hoja ya vijana kupewa hamasa zaidi ili kuepuka maswala kama hayo.
Kauli yao ilishabikiwa na mchungaji Amos Adimile ambaye amewataka wazazi kuwa karibu na wanao kipindi hichi cha likizo ili kuwaepusha na mimba za utotoni.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Young Dreams Halima Alinoor, ambaye amelitaja ongezeko la visa vya mimba za utoto katika eneo hilo kama swala linalofaa kuangaziwa kwa kina.
Halima ametaja kwamba pia ipo haja ya kuangazia maswala ya kuavya mimba kati ya vijana ambalo pia limetajwa kuongezeka katika eneo hilo.