Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Isaac Waihenya,
Mkurugenzi wa shirika la IFPC Hassan Mulata amekanusha madai kwamba kuna baadhi ya vijana waliotegwa katika sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana iliyoandaliwa katika shule ya upili ya Moi Girls hapa mjini Marsabit.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee mulata ambaye alikuwa mmoja wa waandaaji wa hafla hiyo maetaja kwamba kila kijana alialikwa na kuhusishwa kwani matangazo yalifanywa ha kupitia vyombo vya habari.
Mulata amekariri kuwa waandaji wa hafla hiyo walitumia mitandao kuwapata watakaoshirika baadaa yao kujiandikisha.
Aidha Mulata ametaja kwamba baadhi ya maswala yaliyoangaziwa katika wiki hiyo ni ikiwemo jinsi ya kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira.
Kuhusiana na swala la ongezeko la utumizi wa mihadarati kati ya vijana hapa jimboni Marsabit, Mulata ameitaja hoja ya wananchi kushirikiana na asasi za serekali ili kutatua kero hilo.