Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Grace Gumato
Mahakama ya Marsabit imemuhukumu kifungu cha miaka miwili gerezani mwanaume mmoja mwenye umri wa makamu kwa kosa la kupiga na kuumiza mtu.
Mshukiwa Kamau Kamotho anadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 mwezi huu almjeruhi vibaya mlalamishi Adan Isaak wakiwa mjini Marsabit eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.
Mbele ya hakimu Simon Arome mshukiwa alikubali shtaka hilo huku mahakama ikimpa kifungu cha miaka miwili gerezani.
Wakati uo huo washukiwa Isaack Roba na Dub Jillo wamefikishwa mbele ya mahakama ya Marsabit hii leo kwa makosa mawili ambayo ni kosa la wizi na la pili likiwa ni kosa la kumiliki mali iliyoibiwa.
Washukiwa wao wanadaiwa kuwa mnamo tarehe 30 Octoba mwaka 2023 katika eneo la Maata-Arba kaunti ndogo ya Saku kaunti ya Marsabit waliibia bidhaa zinavyogharimu shillingi 283,000 mali ya malalamishi Hassan Noor Boru.
Washukiwa walifikishwa mbele ya hakimu Simon Arome na kukana mashtaka dhidi yao huku mahakama ikiwapata na hatia ya wizi na kuwapa kifungu cha miaka minne gerezani.