Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Samuel Kosgei, Waziri wa afya kaunti ya Marsabit Grace Galmo amesema kuwa wizara yake bado inasubiri ripoti kamili kuhusiana na aina mpya ya mbu hatari waliotambulika katika maeneobunge ya Saku na Laisamis na taasisi ya utafiti wa matibabu chini KEMRI ili waweze kuchukua hatua inayofaa baada ya kushauriwa na[Read More…]
Na Samuel Kosgei, Huenda sasa ikawa afueni kwa wagonjwa katika hospitali za rufaa za Marsabit baada ya serikali kupokea dawa kutoka kwa mamlaka ya kusambaza dawa nchini KEMSA. Akizungumza baada ya kupokea dawa hizo katika hospitali ya rufaa ya Marsabit, waziri wa afya Grace Galmo amesema kuwa dawa hizo zimegharimu[Read More…]
Na Samuel Kosgei, WAWAKILISHI wadi kaunti ya Marsabit wamesema kuwa wako tayari kufanya kazi pamoja na gavana wa sasa Mohamud Ali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Wawakilishi wadi hao wakiongozwa na MCA wa Marsabit Central Jack Elisha wamesema kuwa wakati wa siasa umeisha na kwa ajili ya kufaidi wananchi[Read More…]
Na Samuel Kosgei, MRATIBU mkuu wa mamlaka ya kudhibiti athari za ukame NDMA tawi la Marsabit Mustafa Parkolwa amesema zaidi ya mifugo elfu 300 kaunti ya Marsabit wamekufa kutokana na kiangazi kikali kinachoshuhudiwa kutokana na ukosefu wa mvua kutonyesha kwa misimu mitano. Akizungumza na shajara kwenye kikao cha pamoja cha[Read More…]
Na Isaac Waihenya, Mtoto mmoja kati ya umri wa miaka 5 na 6 ameaga dunia baada ya kuliwa na fisi katika kijiji cha Tirgamo eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit. Akidhibitisha kisa hicho Chifu wa eneo hilo Agostino Supeer ametaja kuwa msichana huyo alitoka nje kujisaidia mida ya usiku[Read More…]
Na Silvio Nangori, Wanafunzi 54 wanaotoka katika familia maskini katika kaunti ya Marsabit na Samburu wamepokea ufadhili wa masomo kupitia shirika lisilo la kiserikali Kenya Drylands Education Fund. Akizungumza na shajara ya jangwani Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Ahmed Kura amesema kwamba waliopata ufadhili huo ni wale wasiojiweza katika jamii.[Read More…]
Na Silvio Nangori, Seneta wa kaunti ya Marsabit Muhamud Chute ametoa wito kwa idara ya usalama kuwakamata wanaoshukiwa kuhusika katika wizi wa chakula unaodaiwa kufanyika katika eneo la sololo eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit. Akizungumza na idhaa hii moja kwa moja Seneta Chute amesema kwamba ni aibu zaidi[Read More…]
Na Isaac Waihenya, Waliohusika katika katika kisa cha wizi wa chakula cha msaada katika eneo la Sololo jimboni Marsabit lazima wachukuliwe hatua za kisheria. Ndio kauli yake naibu kamishina wa kaunti ndogo ya Sololo Robert Nzuki. Akizungunza na vyombo vya habari Nzuki amesema kwamba tayari uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na ripoti[Read More…]
Na Isaac Waihenya, Serekali itahakikisha kwamba wanafunzi wote waliofanya mitihani ya kitaifa ya Gredi ya 6 na KCPE mwaka jana wanaendelea na elimu yao. Kwa mujibu wa kaimu kaunti kamishina wa Marsabit George Kamweru ni kuwa ni haki ya kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa gerdi ya sita kujiunga na Junior[Read More…]
Na Isaac Waihenya, Onyo kali imetolewa kwa wanaopania kuvuruga usalama barabarani haswa katika barabara kuu ya Marsabit kuelekea Isiolo kuwa watakabiliwa kisheria. Kaimu kaunti kamishina wa kaunti ya Marsabit George Kamweru ametoa tahadhari hiyo huku akitaja kwamba ni hatia kisheria kufunga barabara ya umaa au kuendeleza shughuli zote za kihuni[Read More…]