County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Mtoto mmoja aliwa na fisi katika kijiji cha Tirgamo eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit.

Picha;Hisani

Na Isaac Waihenya,

Mtoto mmoja kati ya umri wa miaka 5 na 6 ameaga dunia baada ya kuliwa na fisi katika kijiji cha Tirgamo eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit.

Akidhibitisha kisa hicho Chifu wa eneo hilo Agostino Supeer ametaja kuwa msichana huyo alitoka nje kujisaidia mida ya usiku saa nne unusu na ndipo akabebwa na fisi.

Chifu Supeer ametaja kuwa juhudi za kumuokoa mtoto huyo hazikufua dafu huku mabaki yake yakipatikana baadae.

Aidha Chifu Supeer ametaja kwamba swala la fisi kuwahangaisha wananchi linasababishwa na uwepo wa janga la ukame ambalo liakidhiri katika kaunti nzima ya Marsabit.

Subscribe to eNewsletter