Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
KANISA katoliki jimbo la Marsabit Jumamosi ilisherehekea miaka 60 ya kueneza injili, maadhimisho iliyofanyika kanisa katika kanisa la Cathedral mjini Marsabit.
Misa takatifu iliongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nyeri Anthony Muheria.
Kwenye mahubiri yake Askofu Muheria alisema kuwa ni jukumu la wakristu kusimama kidete katika imani ambayo itawasaidia kupambana na changamoto ya maisha.
Kwenye sherehe hizo zilizosheni mbwembwe na vigelegele Askofu mkuu Muheria alisema kuwa iwapo wakristu wataungana na kusaidia viongozi wa kanisa katika kuboresha huduma ya kanisa kwa wakristu wote, basi hakutakuwepo na tatizo wakati wa kusambaza injili.
Alisema kuwa jimbo hili limekomaa kwa hivyo aliwahimiza wakristu kuinua wakristu wengine wapate kumjua Kristu huku akisisitiza haja ya wakristu kuwa na moyo wa kujitolea.
Kiongozi huyo wa kidini pia aliwataka wakristu kuombeana miito kanisani ili kusaidia katika kuboresha Imani na kueneza injili jimboni bila kukatika.
Aidha Askofu Muheria alitumia mahubiri yake kushukuru mapadre na maskofu wengine wa miaka ya nyuma kama vile Askofu wa kwanza wa jimbo katoliki la Marsabit Charles Cavallera na Askofu Ambrose Ravasi wote waliotoka mbali kuhudumia jimbo hili.
Aliwashukuru kwa kazi yao njema waliofanya.