County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Wanafunzi 54 katika kaunti ya Marsabit na Samburu wapokea ufadhili wa masomo kupitia shirika lisilo la kiserikali Kenya Drylands Education Fund.

Mmoja wa wanafunzi waliofaidika na ufadhili kutoka KDEF.
Picha; Silvio Nangori.

Na Silvio Nangori,

Wanafunzi 54 wanaotoka katika familia maskini katika kaunti ya Marsabit na Samburu wamepokea ufadhili wa masomo kupitia shirika lisilo la kiserikali Kenya Drylands Education Fund.

Akizungumza na shajara ya jangwani Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Ahmed Kura amesema kwamba waliopata ufadhili huo ni wale wasiojiweza katika jamii.

Amesema kwamba ufadhili huo umetolewa ili kuwapa msaada wazazi ambao wamepoteza mifugo wao kufuatia kiangazi ambayo imeshuhudiwa katika maeneo kame.

Wakizungumza na idhaa hii wanafunzi walionufaika wamesema kwamba iwapo shirika la KDEF halingejitokeza kuwapa ufadhili wengi wao wangeishia kusalia nyumbani bila kujiunga na kidato cha kwanza.

Subscribe to eNewsletter