WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Samuel Kosgei,
WAWAKILISHI wadi kaunti ya Marsabit wamesema kuwa wako tayari kufanya kazi pamoja na gavana wa sasa Mohamud Ali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Wawakilishi wadi hao wakiongozwa na MCA wa Marsabit Central Jack Elisha wamesema kuwa wakati wa siasa umeisha na kwa ajili ya kufaidi wananchi baadhi yao wako radhi kusimama na gavana wa sasa.
Wakizungumza mjini Moyale wakati wa uzinduzi wa ufadhili wa masomo kwa watoto Zaidi ya 1000 wawakilishi hao wamesema kuwa hali ya kiangazi imefanya maisha kuwa ngumu kwa wazazi kujilipia karo kutokana na mifugo kufa hivyo wanasema ufadhili kwa ajili ya wanafunzi maskini ni suala la kuchangamkia.
Halkano Sora na Dida Hampicha ni wawakilishi wadi Obbu na Butiye mtawalia.
Mbunge wa Laisamis Joseph Lekuton kwa upande wake alisema kuwa alama zinazotumika kama kigezo cha kuwapa ufadhili watoto zinafaa kuangaliwa upya haswa katika maeneo ya mashinani. Ametaka mca kurekebisha sera hiyo ya kigezo cha alama Zaidi ya 300 ili mwanafunzi asaidiwe.
Aidha ameimba wizara ya elimu na tume ya kuajiri walimu nchini TSC waangazie upya suala la kuongeza idadi ya walimu haswa eneobunge la Laisamis anayodai kuwa shule nyingi hazina walimu wa kutosha.