County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Bado tunasubiri ripoti kamili kuhusiana na aina mpya ya mbu hatari. – Asema waziri wa Afya Grace Galmo.

Na Samuel Kosgei,

Waziri wa afya kaunti ya Marsabit Grace Galmo amesema kuwa wizara yake bado inasubiri ripoti kamili kuhusiana na aina mpya ya mbu hatari waliotambulika katika maeneobunge ya Saku na Laisamis na taasisi ya utafiti wa matibabu chini KEMRI ili waweze kuchukua hatua inayofaa baada ya kushauriwa na serikali kuu.

Anasema hata kabla ya ripoti hiyo tayari walikuwa wametambua visa vipya na ongezeko la malaria jimboni.

Amesema watafiti wa taasisi hiyo ya KEMRI watakua marsabit kwa wiki mzima ili wakamilishe utafiti wao na kupendekeza namna ya kutibu malaria itakayotokana na mbu hao.

Kwa sasa amewataka wananchi wazidi kutumia neti za kuzuia mbu huku wakisubiri utafiti kamili kukamilishwa na watafiti wa afya nchini.

KEMRI mwishoni mwa wiki ilisema kuwa mbu hao kwa jina anopheles stephensi walikuwa wakipatikana sana Kusini mwa bara Asia, Mashariki ya Kati na mataifa ya Uarabuni. Aidha ilisema ishawahi kupatikana katika mataifa ya Djibouti, Ethiopia, Sudan, Somalia na Nigeria miaka ya nyuma.

KEMRI ilisema Uwepo huo itazidisha uwepo wa malaria kwa kasi haswa mijini na vijijini.

Subscribe to eNewsletter