HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya na John Bosco,
Wito unazidi kutolewa kwa wakaazi wa eneo bunge la Laisamis kufuata maagizo ya wizara ya afya ili kujizuia dhidi ya ugonjwa wa malaria baada ya kubainika kwa aina mpya ya mbu wanaoaminika kuwa wabaya.
Kwa mujibu wa chifu wa eneo la Laisamis Agostino Supeer ni kwamba wananchi sio tu wa eneo bunge la Laisamis bali kaunti nzima ya Marsabit wanafaa kulala ndani ya neti ili kujizuia dhidi ya maradhi hayo.
Chifu Agostino ameyasema hayo baada ya waziri wa afya katika kaunti ya Marsabit Bi. Grace Galmo kusema kuwa idara yake inasubiri ripoti kamili kutoka kwa taasisi ya kimatibabu nchini KEMRI ili kuweza kuchukua hatua inayofaa kuhusiana na swala hilo.
Hiyo jana watafiti wa KEMRI ilibaini aina mpya ya mbu maarufu kama Anopheles Stephensi ambao inasemakana kwamba wanasambaa zaidi katika maeneo ya mijini na hata mashinani.