County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Shule 26 katika kaunti ya Marsabit zitanufaika na mradi unaoendeshwa na wizara ya elimu wa kuboresha shule mbambali hapa nchini (SEQIP).

Msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama.
Picha; Radio Jangwani

Na Isaac Waihenya na John Bosco,

Shule 26 katika kaunti ya Marsabit zitanufaika na mradi unaoendeshwa na wizara ya elimu wa kuboresha shule mbambali hapa nchini (SEQIP).

Kwa mujibu wa msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama ni kuwa shule 14 kutoka eneo bunge la Moyale zitanufaika na vyoo 10, maabara 5, madarasa 4, huku maji, darasa moja maalum, na choo kimoja maalum zikijengwa katika shule ya watu wasio na uwezo wa kuskia mjini Moyale, Moyale School for Deaf.

Katika eneo bunge la Laisamis ni shule saba zitakazonufaika na mradi huo ambazo zitajengewa vyoo saba, huku shule 4 zikinufaika katika eneo bunge la Saku kwa kujengewa maabara 3 na madarasa 11 zaidi.

Shule ya Kalacha Nomadic Girls iliyoko eneo la Chalbi ambayo ndio shule pekee kutoka eneo bunge la North Horr katika mradi huo, itanufaika na choo kimoja.

Kwa ujumla kaunti ya Marsabit itapata maabara 8 zaidi, madarasa 15, darasa moja maalum, vyoo 18, pamoja na choo kimoja maalum katika mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwaka huu 2023.

Subscribe to eNewsletter