KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Samuel Kosgei,
MRATIBU mkuu wa mamlaka ya kudhibiti athari za ukame NDMA tawi la Marsabit Mustafa Parkolwa amesema zaidi ya mifugo elfu 300 kaunti ya Marsabit wamekufa kutokana na kiangazi kikali kinachoshuhudiwa kutokana na ukosefu wa mvua kutonyesha kwa misimu mitano.
Akizungumza na shajara kwenye kikao cha pamoja cha wawakilishi wa serikali na washikadau wanaosaidia kupunguza makali ya njaa CSG, Parkolwa amesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya kutokana na tegemeo hilo la wafugaji kupotea.
Aidha anasema kuwa asilimia 98% ya mabwawa na chemichemi za maji zimekauka kutokana na kiangazi kuu inayoshuhudiwa eneobunge la North Horr na Laisamis ikiathirika Zaidi. Msaada Zaidi anasema inahitajika haswa maji na chakula.
Vile vile ameomba wafadhili Zaidi kujitokeza kusaidia wanafunzi kuwalipia karo ya shule kwa kuwa tegemeo lao la kupata karo imeathirika kutokana na ukosefu wa mvua. Zaidi ya watu elfu 300 jimbo la marsabit sawa na asilimia 70 anasema wanahitaji msaada kibinadamu.