Featured Stories / News

MAJAMBAZI WAWILI WA WIZI WA MIFUGO WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAJERAHA YA RISASI BAADA YA KUKABILIANA NA MAAFISA WA POLISI MARSABIT..

Na Caroline Waforo Majambazi wawili wa wizi wa mifugo wamethibitishwa kufariki dunia kutokana na majeraha ya risasi  waliopata wakati wa makabiliano na maafisa wa polisi katika visa viwili tofauti jimboni Marsabit. Ni vifo ambavyo vimethibitishwa na afisa mkuu wa idara ya upelelelezi na jinai jimboni Marsabit Luka Tumbo. Katika kisa[Read More…]

NAIBU GAVANA WA MARSABIT AITAKA JAMII ZA MARSABIT KUACHANA NA TAMADUNI YA WIZI WA MIFUGO AKISEMA INAREJESHA HOFU.

Na Samuel Kosgei  Naibu gavana wa Marsabit Solomon Gubo ameitaka jamii za Marsabit kuachana na tabia na tamaduni zilizopitwa na wakati ikiwemo wizi wa mifugo. Akizungumza kwenye kikao kilicholeta pamoja maafisa wa idara ya Utalii na Utamaduni na Taasi ya kitaifa ya makavazi, Gubo alisema bado kuna tamaduni nzuri zilizosalia[Read More…]

Tamaduni na mila za jamii za Marsabit sasa kuhifadhiwa kidijitali kwa ajili ya kizazi kijacho.

. Na Samuel Kosgei   Serikali ya kaunti ya Marsabit ikishirikiana na Taasisi ya makavazi za kitaifa National Museum Of Kenya (NMK) imeweka makubaliano ya kushirikiana kuweka utamaduni na mila za jamii 10 asilia za Marsabit katika hifadhi ya kidigitali kinyume ilivyo Kwa Sasa ambapo tamaduni hizo hazijahifadhiwa kidigitali. Waziri wa Utalii[Read More…]

WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA MARSABIT WALIOHUDUMU BILA MALIPO ENZI YA CORONA WALALAMA KUTOAJIRIWA NA SERIKALI YA KAUNTI.

  Na Lelo Wako Vijana waliojitolea kutoa huduma hospitalini katika kaunti ya Marsabit miaka sita iliyopita wameonesha masikitiko yao ya kutoajiriwa na serikali ya kaunti hata licha ya wao kutoa huduma za afya bila mshahara kutoka mwaka wa 2018. Vijana hao wakizungumza mjini Marsabit wameonesha masikitiko yao huku wakieleza kuwa[Read More…]

Wakaazi kaunti ya Isiolo wafanya maandamano ya Amani kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024.

NA CAROLINE WAFORO Wakaazi kaunti ya Isiolo wamefanya maandamano ya Amani kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024. Wakaazi hao an ambao idadi kubwa ni vijana wamesema mswada huu unalenga kuwakadamiza wakenya ambayo tayari wanakabiliwa na mzigo mzito wa kiuchumi. Waandamanaji hao wamesema kuwa hawajaona manufaa ya ushuru ambao[Read More…]

Wakaazi wa Marsabit watakiwa kuwasilisha malalamishi yoyote kuhusu vitambulisho kwa ofisi ya usajili wa vitambulisho Jimboni, chifu au DCC.

Na caroline Waforo Wakaazi wa Kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwasilisha malalamishi yoyote ya vitambulisho kwa ofisi ya usajili wa vitambulisho Jimboni, ofisi ya chifu au hata afisi ya mkuu wa wilaya yaani DCC. Ni wito ambao umetolewa na Michael Rapolo ambaye ni mkuu wa usajili wa watu jimboni Marsabit na[Read More…]

MASHINDANO YA MICHEZO YA MUHULA WA PILI YA SHULE ZA UPILI KITENGO CHA KAUNTI NDOGO YAMEANZA NA YANAENDELEA KATIKA ENEO BUNGE LA SAKU.

NA JOHN BOSCO NATELENG Mashindano ya michezo ya Muhula wa pili ya shule za upili kitengo cha kaunti ndogo yameanza na yanaendelea katika eneo bunge la Saku. Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo katika shule ya upili ya Moi Girls, Mkurugenzi wa elimu wa kaunti ndogo ya Saku Hussein Harubu amesema kuwa[Read More…]

Subscribe to eNewsletter