Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Caroline Waforo
Majambazi wawili wa wizi wa mifugo wamethibitishwa kufariki dunia kutokana na majeraha ya risasi waliopata wakati wa makabiliano na maafisa wa polisi katika visa viwili tofauti jimboni Marsabit.
Ni vifo ambavyo vimethibitishwa na afisa mkuu wa idara ya upelelelezi na jinai jimboni Marsabit Luka Tumbo.
Katika kisa cha kwanza wahalifu walikabiliana na maafisa wa polisi wakati wa jaribio la wizi wa mifugo zaidi ya 200 katika eneo la Badassa na ambayo maafisa wa polisi walifanikiwa kuwarejesha.
Aidha hapo jana usiku wa saa sita polisi walifanikiwa kumkamata moja wa wezi hao wa mifugo alipokuwa amepelekwa na wenzake kutafuta matibabu katika kliniki moja eneo la Karare baada ya kupigwa risasi mkono wa kulia huku pia akithibitishwa kuvunjika mkono huo.
Mahabusu huyo yupo katika hospitali ya rufaa ya Marsabit akisubiri kupewa rufaa hadi katika hospitali nyingine kwa matibabu.
Aidha daktari aliyekuwa amshughulikie mhalifu huyo bado anaendelea kuzuiliwa akisubiri kuhojiwa.
Katika kisa hicho ng’ombe 12 walipigwa risasi wakati wa makabilianao huku ng’ombe moja akifariki kutokana na majeraha.
Katika kisa cha pili mhalifu moja alifariki dunia kutokana na majeraha aliopata wakati wa makabiliano baina yao na maafisa wa polisi.
Hii ni baada ya uvamizi wa gari moja la uchukuzi la kampuni ya Meiso usiku wa kuamkia Jumapili katika barabara ya Hulahula-Kargi
Afisa mkuu wa idara ya upelelelezi na jinai jimboni Marsabit Luka Tumbo amewataka wananchi kuendelea kutoa ripoti muhimu kwa idara ya usalama huku akiweka wazi kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kuwakamata wahalifu wote waliohusika na visa hivyo.