Local Bulletins

Wakaazi kaunti ya Isiolo wafanya maandamano ya Amani kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024.

NA CAROLINE WAFORO

Wakaazi kaunti ya Isiolo wamefanya maandamano ya Amani kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024. Wakaazi hao an ambao idadi kubwa ni vijana wamesema mswada huu unalenga kuwakadamiza wakenya ambayo tayari wanakabiliwa na mzigo mzito wa kiuchumi.

Waandamanaji hao wamesema kuwa hawajaona manufaa ya ushuru ambao wakenya wamekuwa wakitozwa kuambatana na sharia ya fedha ya  waka 2023.

Wakati uo huo wamewataka wabunge wa Isiolo akiwemo Mumina Bonaya, Joseph Samal na Mohammed Tupi kupiga kura ya kupinga mswada huo bungeni

Subscribe to eNewsletter