Featured Stories / News

IDARA YA AFYA KAUNTI YA MARSABIT KUAANZA KUWAFANYIA UCHUNGUZI WA HOMA YA NYANI YA MPOX WASAFIRI WOTE WANAOINGIA JIMBONI…

Na Caroline Waforo. Idara ya afya kaunti ya Marsabit itaanza kuwafanyia uchunguzi wa homa ya nyani ya MPOX wasafiri wote wanaoingia jimboni. Hii ni kutokana na kuendelea kurekodiwa kwa ugonjwa huo wa MPOX humu nchini pamoja na kisa kinachoendelea kufanyia uchunguzi katika kaunti jirani ya Isiolo. Kulingana na afisa wa[Read More…]

MAKUNDI YANAYOFANYA BIASHARA YA UPANZI WA MICHE KAUNTI YA MARSABIT YATAKIWA KUJIANDIKISHA NA IDARA YA MISITU ILI KUNUFAIKA NA MIPANGO YA SEREKALI.

Na Isaac Waihenya,  Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kutunza miche ambayo imepandwa ili kuongezea kiwango cha miti hapa jimboni. Kulingana wa afisa mkuu katika idara ya misitu na mali asili kaunti ya Marsabit Pauline Marleni aliyeongea na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee,ni kwamba iwapo jamii haitatunza miche iliyopandwa[Read More…]

WAKAAZI WA MARSABIT WATOA MAONI TOFAUTI KUHUSIANA NA MAPENDEKEZO YA KUUNDWA KWA OFISI YA KIONGOZI WA UPINZANI.

Na Talaso Huka Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia mseto kuhusu pendekezo la kuundwa kwa afisi rasmi ya kiongozi wa upinzani. Baadhi ya waliozungumza na Radio Jangwani wameunga mkono pendekezo hilo wakisema kuwa kuundwa  kwa ofisi rasmi ya upinzani itasaidia katika kuwajibisha serikali Hata hivyo mmoja wa mkaazi ameonekana kupinga[Read More…]

DARA YA UVUVI MARSABIT YATAKIWA KUWEKA MIKATATI ITAKAYOSAIDIA UCHUKUZI KATIKA ZIWA TURKANA NA KUPUNGUZA AJALI ZA MASHUA KATIKA ZIWA HILO.

Na JohnBosco Nateleng’ Wito umetolewa kwa serekali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya uvuvi imetakiwa kuweka mikatati ambayo itakuwa ikilinda uchukuzi unaoendelea katika ziwa Turkana ili kuweza kupunguza ajali za mashua zinazoshuhudiwa katika ziwa hilo. Kwa mujibu wa aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha MCA wadi wa Loiyangalani na ambaye[Read More…]

WAKAAZI WA MARSABIT WANAOISHI KARIBU NA MISITU WATAKIWA KUKOMA KULISHA MIFUGO YAO NDANI YA MSITU HADI WAKATI WA KIANGAZI.

Na Talaso Huka Wakaazi wa Marsabit wanaoishi karibu na misitu wameshauri kukoma kulisha mifugo yao ndani ya msitu hadi wakati wa kiangazi. Akizungumza na Radio Jangwani Naibu msisamizi wa idara ya msitu Kadiro Oche amewataka wafugaji kuzidi kutumia nyasi zilizopo malishoni mwanzo kabla ya kuvamia misitu kwa ajili ya malisho.[Read More…]

MADAKTARI MARSABIT WATISHIA KUGOMA IWAPO MALALAMISHI YAO HAYATASHUGHULIKIWA CHINI YA WIKI 2.

Na Caroline Waforo Serikali ya kaunti ya Marsabit ina wiki mbili kuanzia leo tarehe 27 mwezi Agosti, kushughulikia matakwa yaliyoibuliwa na madaktari wa kaunti ya Marsabit. Kwenye barua iliyotiwa sahihi na katibu wa KMPDU ukanda huu wa mashariki Dr Elvise Mwandiki madaktari watalazimika kushiriki mgomo iwapo maswala yao hayatasuluhishwa chini[Read More…]

Subscribe to eNewsletter