Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
NA CAROL WAFORO
Mwanaume mmoja amefikishwa mahakamani kwa jaribio la kumbaka mtoto wa miaka 7.
Inakisiwa kuwa mnamo tarehe 7 mwezi February 2024 katika mtaa wa Jaldesa wadi ya Marsabit central kaunti ya Marsabit mshukiwa kwa jina Guyo Kose Duba alitekeleza unyama huo.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 8 mwezi huo wa February na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 12 mwezi uo huo.
Mbele ya hakimu Christine wekesa mshukiwa alikanusha shtaka dhidi yake na kupewa bodi ya shilingi 200,000 ambayo alishindwa kuwasilisha mahakamani.
Kesi hiyo umekuwa ikiendelea huku ikitarajiwa kutajwa tena 11 mwezi septemba mwaka huu wa 2024 na kusikilizwa 1 mwezi wa oktoba.