Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Samuel Kosgei
IDARA ya kilimo kaunti ya Marsabit imewataka wakulima katika sehemu za ukulima kaunti hii wazidishe maandalizi yao ya kupanda ili kuepuka kupatwa ghafla na mvua.
Afisa wa kilimo katika kaunti ya Marsabit Dub Nura akizungmza na shajara amewataka wakulima kuanza kulima mashamba yao ili wawe tayari kupanda chakula pindi mvua zitakapoanza mwezi wa 10 hadi mwezi wa Disemba.
Nura amekiri kuwa ukosefu wa lishe na chakula ambao umeanza kushuhudiwa jimboni kwa sasa imechangiwa na maandalizi duni ya wakulima licha ya mvua kunyesha mapema mwezi wa nne mwaka huu.Anasema iwapo maandalizi ya mashamba na mbegu yatafanyika kwa mapema basi uzalizashaji wa chakula utakuwa juu.
Mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa jimboni Marsabit Abdi Dokata amesema kuwa mvua kiasi inatarajiwa kushuhudiwa katika msimu wa mvua chache za mwezi wa 10 hadi 12.
Baadhi ya nyanda za juu kauti ya Marsabit anasema itapokea mvua kiasi haswa maeneo ya Marsabit Central na sehemu za Moyale. Mvua hizo hata hivyo anasema haitakuwa nyingi kama msimu uliopita.
Mvua hizo chache anasema zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi wa 10 au wiki ya kwanza wa mwezi November na kukamilika wiki ya kwanza ya mwezi wa 12 kama anavyoarifu Abdi Dokata.