Local Bulletins

NAIBU GAVANA WA MARSABIT AITAKA JAMII ZA MARSABIT KUACHANA NA TAMADUNI YA WIZI WA MIFUGO AKISEMA INAREJESHA HOFU.

Na Samuel Kosgei

 Naibu gavana wa Marsabit Solomon Gubo ameitaka jamii za Marsabit kuachana na tabia na tamaduni zilizopitwa na wakati ikiwemo wizi wa mifugo.

Akizungumza kwenye kikao kilicholeta pamoja maafisa wa idara ya Utalii na Utamaduni na Taasi ya kitaifa ya makavazi, Gubo alisema bado kuna tamaduni nzuri zilizosalia katika jamii za Marsabit ambazo zinafaa kuendelezwa ikiwemo mavazi, upishi, nyimbo Kati ya nyingine nyingi.

Anasema kuwa utamaduni wa kuiba mifugo ulipitwa na wakati, hivyo inafaa kutupiliwa mbali.

  Gubo pia amewataka vijana kutosahau mila zao nzuri ikiwemo lugha ya mama ambayo isipolindwa anasema huenda ikapotea miaka ijayo.

Wakati uo huo ameiomba Taasisi inayoshughulikia makavazi na toradhi za kitaifa kuzidi kushirikiana na serikali ya kaunti katika kuimarisha sekta ya Utalii na tamaduni na licha ya kugatuliwa.

Subscribe to eNewsletter