Local Bulletins

Wakaazi wa Marsabit watakiwa kuwasilisha malalamishi yoyote kuhusu vitambulisho kwa ofisi ya usajili wa vitambulisho Jimboni, chifu au DCC.

Na caroline Waforo

Wakaazi wa Kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwasilisha malalamishi yoyote ya vitambulisho kwa ofisi ya usajili wa vitambulisho Jimboni, ofisi ya chifu au hata afisi ya mkuu wa wilaya yaani DCC.

Ni wito ambao umetolewa na Michael Rapolo ambaye ni mkuu wa usajili wa watu jimboni Marsabit na ambaye amezungumza na shajara ya radio Jangwani kwa njia ya kipekee.

Haya ni kutokana na malalamishi ibuka kuhusu mkanganyiko wa majina pamoja na lokesheni.

Aidha amewaonya wakaazi jimboni dhidi ya kutuma maombi ya Vitambulisho vya Kitaifa zaidi ya moja.

Kadhalika amewaonya watu wanaojidai kuwa wafanyikazi wa afisi ya usajili wa vitambulisho na kuwahadaa wakaazi akisema kuwa watachukuliwa hatua kali.

Na huku ikitiliwa maanani kuwa serikali iliondoa uhakiki unaofanyika wakati wa mchakato wa kutuma maombi ya Vitambulisho vya Kitaifa kwa wananchi walio mipakani na wanaotoka baadhi ya makabila fulani madogo nchini  Michael amewaeleza wakaazi vigezo hitajika vya kutuma maombi ya vitambulisho kwa sasa.

Subscribe to eNewsletter