KEWOPA yapendekeza kurejeshwa kwa viboko shuleni kukabiliana na utovu wa nidhamu.
Na JB Nateleng
Muungano wa Wanawake Wabunge nchini (KEWOPA) umependekeza kurejeshwa kwa adhabu ya viboko shuleni kama njia ya kukabiliana na ongezeko la utovu wa nidhamu, migomo na visa vya moto vinavyoshuhudiwa katika baadhi ya taasisi za elimu nchini.
Pendekezo hilo linajiri wakati zaidi ya shule kumi zimefungwa kutokana na misururu ya migomo na matukio ya vurugu yaliyosababisha usumbufu wa masomo katika sehemu mbalimbali za nchi.
Viongozi hao wanasema kuna haja ya kutafuta mbinu madhubuti za kurejesha nidhamu shuleni huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya walimu, wazazi na serikali katika kuwalea wanafunzi.
Hata hivyo, suala la kurejeshwa kwa viboko limeendelea kuzua mjadala miongoni mwa wadau wa elimu, huku baadhi wakipendekeza matumizi ya mbinu mbadala za nidhamu zinazozingatia haki za watoto.



Post Comment