Naomi Waqo awawezesha vikundi vya North Horr kiuchumi
Na Nyabande Orwa
Kama njia moja ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Marsabit, Naomi Waqo Jilo, amegawa zana za kazi, vifaa na mtaji wa kuanzisha biashara kwa vikundi mbalimbali vya jamii katika eneo la North Horr.
Walionufaika walipokea vifaa vya biashara, mahema na viti, mashini za kuchomelea vyuma, mizinga ya ufugaji wa nyuki, kati ya vitu vingine vya kusaidia kuanzisha biashara.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naomi Waqo alisema lengo la mpango huo ni kuwapatia wananchi ujuzi na vifaa vitakavyowasaidia kuanzisha au kupanua biashara zao, kujiajiri na kuongeza kipato cha familia.
Mwakilishi huyo wa wanawake alisisitiza kuwa ataendelea kuunga mkono wanawake na vijana kupitia miradi ya ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi ili kujenga jamii inayojitegemea na kuboresha maisha ya wakazi wa Kaunti ya Marsabit.



Post Comment