Serikali kuanza ukarabati wa barabara ya Badassa–Dirib Gombo
Na Nyabande Orwa
Serikali imeanza mchakato wa kukarabati barabara ya Badassa–Dirib Gombo, siku moja baada ya wakazi wa maeneo hayo kuwasilisha malalamiko yao kuhusu ubovu wa barabara hiyo kwa ofisi ya kamishna wa kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na Shajara katika ofisi yake hii leo, kamishna, Stanley Kamande, amesema maandalizi ya ukarabati tayari yameanza na mkandarasi yuko tayari kuanza kazi katika barabara hiyo.
Kamande amewataka wakazi kuwa na subira huku serikali ikiendelea na hatua za kuhakikisha ukarabati wa barabara hiyo unatekelezwa kwa haraka.



Post Comment