Highlights

Serekali yatakiwa kuimarisha haki ya elimu kwa watoto wanaoishi na ulemavu Marsabit

Na JB Nateleng

Watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Marsabit bado wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kupata elimu kutokana na ukosefu wa miundombinu inayokidhi mahitaji yao pamoja na uhaba wa vifaa maalum vya kujifunzia.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Shirika la World Vision Marsabit, James Jarso, baadhi ya watoto wanaoishi na ulemavu hawapati fursa ya kuhudhuria masomo kwani shule nyingi katika kaunti ya Marsabit  hazijaandaliwa ipasavyo kuwahudumia watoto wenye ulemavu.

Vilevile, Jarso ameeleza kuwa bado kuna uelewa mdogo katika jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto wanaoishi na ulemavu shuleni, akitoa wito kwa idara husika kuimarisha kampeni za uhamasishaji kuhusu haki za watoto hao.

Aidha, ametaja uhaba wa walimu wenye ujuzi wa lugha ya ishara pamoja na elimu maalum kuwa miongoni mwa changamoto zinazokwamisha juhudi za kuhakikisha watoto wanaoishi na ulemavu wanapata elimu bora na jumuishi.

Jarso ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa, viongozi wa kidini na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu kushirikiana katika kuwekeza kwenye miundombinu na huduma muhimu zitakazowezesha watoto wanaoishi na ulemavu kupata fursa sawa za elimu, maendeleo na ushiriki kamili katika jamii.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Shanon

You actually make it seem so easy with your presentation but I find this matter to be actually
something that I think I would never understand. It seems too complicated and extremely broad for me.

I am looking forward for your next post, I will try to get the
hang of it!

Post Comment