Askofu Chaima wa Malawi asema vijana ni nguzo muhimu ya kanisa.
Askofu wa Jimbo katoliki la Zomba nchini Malawi, Rt. Rev. Alfred Mateyu Chaima, amelikumbusha kanisa kwamba vijana hawawezi kuchukuliwa kama watu wa pembeni katika maisha na utume wa Kanisa.
Akizungumza wakati wa kikao cha vijana katika mkutano mkuu wa 21 wa AMECEA, Askofu Chaima amesisitiza kuwa kanisa haiwatengi vijana, bali inawatambua kama sehemu muhimu ya familia ya Mungu.
Kauli hiyo inakuja wakati ambapo vijana katika nchi wanachama wa AMECEA wanazidi kutoa wito wa kujumuishwa zaidi, kushirikishwa kikamilifu na kusindikizwa katika maisha ya Kanisa.
Aidha, ametoa wito kwa parokia na jumuiya za Kikristo kuondokana na mtazamo wa kuwaalika vijana kwenye shughuli za Kanisa pekee.



Post Comment